Russia yashambulia Lviv na Kyiv ikitishia Kutumia Makombora ya Masafa Marefu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanajeshi wa Ukraine akitumia silaha wakati wa mazoezi ya kijeshi huko Lviv region
Mwanajeshi wa Ukraine akitumia silaha wakati wa mazoezi ya kijeshi huko Lviv region
Ndege za kivita za Russia zimepiga mabomu Lviv na makombora yake yamepiga pia Kyiv Jumamosi, wakati Moscow ikiendeleza vitisho vya kushambulia kwa makombora ya masafa marefu katika miji mbalimbali ya Ukraine baada ya meli yake maalum ya kivita kuzamishwa katika bahari ya Black Sea.

Ndege za kivita za Russia zimepiga mabomu Lviv na makombora yake yamepiga pia Kyiv Jumamosi, wakati Moscow ikiendeleza vitisho vya kushambulia kwa makombora ya masafa marefu katika miji mbalimbali ya Ukraine baada ya meli yake maalum ya kivita kuzamishwa katika bahari ya Black Sea.

Katika mji uliozingirwa wa Mariupol, eneo lenye mapigano makali katika viti hivi na janga baya sana la kibinadamu, majeshi ya Russia yameweka shinikizo la kusonga mbele na mashambulizi, wakitarajia kufidia kwa kushindwa kuikamata Kyiv na hatimaye kupata zawadi yao ya kwanza kubwa ya vita hivi.

Moscow imesema ndege zake zimeshambulia kiwanda cha kukarabati vifaru katika mji mkuu, ambako mlipuko ulisikika na moshi ulionekana katika wilaya ya Darnystskyi iliyoko kusini mashariki. Meya wake alisema waokoaji na madaktari walikuwa wako kazini huko lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.


Jeshi la Ukraine lilisema ndege za kivita za Russia zilizokuwa zimeruka kutoka Belarus zilipiga makombora katika mkoa wa Lviv karibu na mpaka wa Poland, ambako makombora yalitunguliwa na ulinzi wa anga wa Ukraine.

PandKote nchini Ukraine hadi kusini mashariki huko Mariupol, waandishi wa habari wa Reuters katika maeneo yanayoshikiliwa na Russia ya mji wa bandari walifika katika eneo la shughuli za chuma za Ilyich, ambayo Moscow ilikuwa imedai imekikamata Ijumaa, moja ya viwanda viwili vikubwa vya chuma ambako walinzi wamejificha katika madaraja na mahandaki ya chini ya ardhi.

Kiwanda hicho kimeharibiwa na kuwa ni ghofu lenye vyuma vilivyopinda na zege lililopasuka, na hakuna alama ya waliokuwa wanalinda kuwepo.


Nje, kiasi cha nusu darzeni ya miili ya raia ilikuwa imetawanyika katika mitaa ya karibu, ikiwemo mwanamke mwenye nguo ya pinki na viatu vyeupe.

Kuna mtu alikuwa amechora kwa rangi “neno mined” katika ukuta upande wa uwanja wa mbele wa kituo cha mafuta kilichokuwa kimeharibiwa. Ikiwa ni nadra kuona alama ya uhai, gari moja jekundu lilikuwa inapita polepole katika mtaa uliokuwa mtupu, neno “watoto” lilikuwa limeandikwa katika kadi iliyokuwa imebandikwa kwa gundi kwenye kioo cha mbele cha gari.

Huko Mykolaiv, mji mwingine ulioko karibu na mstari wa mbele huko kusini, Russia imesema ilikuwa imekishambulia kiwanda cha kukarabati magari ya kijeshi.

Mashambulizi ya mabomu na makombora yamefuatia tangazo la Russia Ijumaa kuwa itaendeleza zaidi mashambulizi ya masafa marefu kwa kulipiza kisasi dhidi vitendo vya “hujuma” na “ugaidi” ambavyo havijafafanuliwa saa kadhaa baada ya kuthibitisha kuzama kwa meli yake ya kitaifa Moskva katika bahari ya Black Sea.


Kyiv na Washington wanasema meli hiyo ilipigwa na makombora ya Ukraine, shambulizi linaloonyesha mafanikio ya Jeshi la Ukraine dhidi ya adui mwenye silaha bora zaidi. Moscow inasema meli hiyo ilizama baada ya kushika moto.

Mwezi mmoja na nusu wa uvamizi unaofanywa na Rais Vladimir Putin huko Ukraine, Russia inajaribu kukamata eneo upande wa kusini na mashariki baada ya kujiondoa upande wa kaskazini kufuatia mashambulizi makubwa dhidi ya Kyiv yaliyozimwa katika maeneo nje ya mji mkuu.

Majeshi ya Russia yalijiondoa kutoka kaskazini wakiiacha miji ikiwa na miili ya raia iliyotawanyika, ushahidi wa kile Rais wa Marekani Joe Biden wiki hii alikiita mauaji ya kimbari – jaribio la kutaka kufuta kabisa utaifa wa Waukraine.

Russia imekanusha kulenga raia na inasema lengo ya kile inachokiita ni “operesheni maalum ya kijeshi” ni kuwanyang’anya silaha, kuwashinda wazalendo na kuwahami waliowachache katika eneo la kusini mashariki.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad