Kiungo Bruno Fernandes anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Manchester United kitakachoivaa Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, licha ya kuhusika kwenye ajali ya gari lake ambayo ilitokea mapema hii leo.
Kiungo wa Man United, Bruno Fernandes akionekana kwenye ajali iliyotokea mapema leo.
Imearifiwa kuwa nyota huyo alipata ajali ingawa hakuumia na alijumuika na wenzake mazoezini wakiwa wanajiwinda na mchezo wa kesho.
'
Akizungumzia hali ya mchezaji huyo Kocha wa Man United, Ralph Rangnick amesema''Ni kweli amefanya mazoezi na kikosi, ajali ilitokea Carringhton ,na ninachofahamu hakuna aliyeumia hivyo bila shaka kesho atakuwepo kwa ajili ya mechi yetu.''
Man United inaisaka nafasi ya kumaliza ndani ya nne bora ambapo hadi sasa wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 54 baada ya michezo 32, watakabiliana na Liverpool walio katika nafasi ya pili wakifukuzana na Manchester City kwenye kuusaka ubingwa wa EPL.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA