4/09/2022

Urusi imembadilisha kamanda wake wa vita, afisa wa Magharibi athibitisha
Afisa wa magharibiamethibitisha kuwa Urusi imepanga upya uongozi wa operesheni zake za kivita katika Ukraine, na kumteua Jenerali mpya mwenye uzoefu wa mapambono ya kivita katika Syria kusimamia vita vya Ukraine.

Akizungumza mwandishi wa BBC Gordon Corera kwa sharti kwamba asitajwe jina lake, chanzo cha taarifa hii kilisema kuwa kamanda wa wilaya ya kijeshi ya kusini mwa Urusi, Jenerali Alexander Dvornikov, sasa ndiye anayeoongoza uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

“Kamanda huyo ana uzoefu mkubwa wa operesheni za Urusi nchini Syria. Kwahiyo tunamtarajiauongozi na udhibiti utaboreka ,” kilisema chanzo hicho.

Uteuzi mpya ulifanyika katika jaribio la kuimarisha uratibu baina ya vikosi mbali mbali , kwani makundi ya Urusi yamekuwa yakipangwa na kuongozwa na wakuu tofauti, alisema afisa.


 
Urusi hadi sasa inahangaika kufikia malengo yake ya kivita, ikishindwa kuichukua miji muhimu kama vile Kyiv kabla ya hatimaye kuelekeza macho yake katika jimbo la Donbas mashariki.

Afisa huyo alisema kuwa mbinu za Urusi zimekuwa zikiwafanya warudishwe nyuma na vikosi vyenye askari wachache wa Ukraine wanaopigana kwa akili zaidi na kwa kushitukiza-licha ya Urusi kufikiriwakuwaina kikosi "kikubwa" chenye bataliani 100 zenye wanajeshi wenye ujuzi.

“Bila kubadili mbinu zake ni vigumu sana kwa Urusi kufanikiwa kwa malengo yao waliyojiwekea wenyewe ," alisema afisa huyo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger