Ticker

6/recent/ticker-posts

Slovakia yaipatia Ukraine mfumo wa kujilinda na makombora chapa S-300

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>Waziri Mkuu wa Slovakia Eduard Heger amearifu kuwa nchi yake imeipatia Ukraine mfumo wa kujilinda na makombora chapa S-300 lakini amesema hatua hiyo haina maana kuwa Slovakia imejiunga kwenye mzozo na Urusi. 

Heger ametoa matashi hayo wakati akiwa ziarani nchini Ukraine pamoja na viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya ambao kwa pamoja wamepangiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky baadae hii leo. 

Maombi ya kupatiwa mfumo huo wa S-300 yalitolewa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita na Rais Zelensky alipowahutibia wabunge wa Marekani akisema ungeisaidia Ukraine kuifunga anga yake dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments