Uzinduzi The Royal Tour Arusha… Wema Atamba “Tumerudi Enzi Zetu za Filamu”Wema Isaac Sepetu siku hizi wanamuita Last Born (Kitindamimba au Mziwanda) wa Taifa; ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Movies ambao jana wameshuhudia uzinduzi wa kishindo wa Filamu ya The Royal Tour na kutoa yake ya moyoni, IJUMAA lilikuwepo eneo la tukio.

Baada ya uzinduzi wa filamu hiyo ya kiwango cha Dunia kuzinduliwa jijini New York na Los Angeles nchini Marekani na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mhusika mkuu, jana Alhamisi ya Aprili 28, 2022 ilikuwa ni zamu ya jijini Arusha ambapo kulikuwa na mtikisiko wa aina yake ndani ya Kituo cha Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

MAMA SAMIA AMEFUNGUA DUNIA

Kufuatia kishindo hicho, Wema ameliambia Gazeti la IJUMAA kwamba, tukio hilo ni chachu ya kuirejesha tasnia ya filamu nchini Tanzania kwenye kilele chake kwani Mama Samia ameshawafungulia Dunia kupitia Filamu ya The Royal Tour.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Wema anasema kuwa, mashabiki wa filamu za Tanzania au Bongo Movies, sasa wanakwenda kuishuhudia tasnia hiyo ikirudi kwenye enzi zake zile za matukio juu ya matukio.


 
“Hii ni wake up call (simu ya kuwaamsha usingizini) kwetu kama tasnia ya filamu kwa sababu Mama (Samia) ameshafungua milango kote duniani.

“Hivi sasa macho na masikio ya wengi ni Filamu ya The Royal Tour na hii itakuwa ni mwanzo mzuri wa watu wa mataifa mbalimbali kufuatilia filamu zetu.

“Mimi naamini Mama ametuonesha kwamba hata filamu za kutangaza vivutio vyetu zinavutia watu wengi kutufuatili na kuzinunua kwa sababu mataifa mengine hawana.


SASA HAKUNA KUPOA

“So (kwa hiyo) watu wategemee filamu za aina hii kutoka kwetu kwa sababu hakuna kupoa tena.

“Sawa, mtu mwingine anaweza kusema sasa Bongo Movies imefufuka na tumerudi kwenye enzi zetu,” anasema Wema.

Akizungumzia kundi lao jipya la mastaa wa Bongo Movies linalokwenda kwa jina la The Big Six likimjumuisha yeye (Wema), Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Kajala Masanja, Aunty Ezekiel na Elizabeth Michael au Lulu anasema wana mipango na mikakati mikubwa ya kufanya makubwa.

“Tunaweza kufanya mambo makubwa sana na nina imani tutafanya kwa sababu tuna mipango mingi na mikakati yetu pia ni mikubwa,” anasema Wema ambaye enzi zake alikuwa hakaukiwi na matukio na alikuwa kivutio kikubwa kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania na kuongeza;


 
“Watu wakae mkao wa kula na wajue mambo mazuri hayaitaji haraka kwani sasa tumefufuka upya.”

ANGUKO LA BONGO MOVIES

Mara tu baada ya kufariki dunia kwa aliyekuwa kinara wa tasnia hiyo, marehemu Steven Kanumba siku ile ya Aprili 7, 2012, zilianza kuibuka dhana kwamba jamaa huyo aliondoka na Bongo Movies yake na ndilo likawa anguko la tasnia hiyo.

Hata hivyo, wapo baadhi ya mastaa wa tasnia hiyo ambao walisema kuwa, kiuhalisia kilichowamaliza Bongo Movies awali ni kukosa dira na kupenda kudandia vitu vya dezodezo ili wapate kipato tofauti na ilivyokuwa kwa Kanumba ambaye alikuwa anafanya jitihada kwenye filamu na kuweka malengo makubwa.

Ilisemekana kuwa, waliobaki, wengi wao walipoteza mwelekeo ndiyo maana wakawa wanakusanywa tu kama mafungu ya nyanya na kupelekwa kwenye siasa bila kujua wanawagawa mashabiki wao.


Zipo skendo nzito ambazo ziliwahusu wale wa kike ambapo ilidaiwa kwamba, walikuwa wanauzwa na kujiuza kwa vigogo na wenye pesa hasa wauza madawa ya kulevya na kugeuza tasnia hiyo kuwa genge la wadangaji, makahaba na makuwadi.

KUFUFUKA KWA BONGO MOVIES

Kwa mujibu wa Wema, tasnia hiyo sasa imefufuka na imeanza upya safari ya kurudi ilipokuwa enzi hizo yapata miaka kumi iliyopita kwa sababu badala ya kwenda mbele ilikuwa ikirudi nyuma.

Stori; Imelda Mtema, Dar

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad