4/21/2022

Yanga Waitangazia Maumivu NamungoWAKATI Yanga ikitarajiwa kuikabili Namungo keshokutwa Jumamosi Uwanja wa Mkapa, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze ametamba kuwa wamejipanga kutumia mfumo wao mpya kwenye safu ya ushambuliaji.

Kocha huyo amezungumza na Spotileo na kuelekeza kuwa amefuatilia mechi za timu hizo mbili na kubaini kuwa mbinu zao zimekuwa zikifanana, ndio maana matokeo yalikuwa sare, hivyo wameona watumie mfumo mpya ambao utawachanganya wapinzani wao.

"Tumedhamiria ubingwa msimu huu, ndio maana tumekua na mikakati mingi, ambayo itatuwezesha kupata pointi tatu na kuvunja mwiko wa kutopata ushindi dhidi ya Namungo," amesema Kaze.

Pia amesema watawashangaza Namungo kwa kasi watakayoanza nayo, lengo likiwa ni kupata mabao mengi mapema na pia wataendelea na kasi hiyo kwa dakika nyingine za mchezo.


Amesema Yanga imepania kumaliza mchezo kipindi cha kwanza na kwamba kama wakiamua kucheza mpira wao wa kawaida watasumbuka na wapinzani wao.


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger