5/22/2022

Ali Kamwe "Mambo 10 nilioyaona GEITA VS SIMBA"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA1 : WHAT A MATCH. CLASSIC! BURUDANI IMEPATIKANA NDANI YA CCM KIRIMBA. ilikuwa mechi kali ya Kibabe, kasi, mbinu ufundi ulitawala. Ahsante Geita Gold kwa Ushindani wa kikubwa✊


2 : GEITA walikuja na 4 - 4 - 2 kama kawaida yao. Wakishambulia kwa mapana ya uwanja. Pablo akarejea na Mfumo wa 4 -3 -3


3. WELL DONE Fred Felix Minziro🙌 kwa kile ambacho anakifanya kwenye kikosi chako. Inaweza kuonekana ndoto Lakini GEITA NI KAMA WAMEANZA KUAMINI KUNA TIKETI YAO YA KIMATAIFA MSIMU UJAO


4. SIMBA walianza mechi vyema Kipindi cha kwanza. Kibu Dennis akitegemea mapafu yake kuisukuma Geita kwenye eneo lao! KUKATA KWA SAKHO ni kama kulianza kuikata system ya Simba


5. Pressing ya Simba ilikuwa bora sana kipindi cha kwanza Namna Kanoute na Bwalya walivyokuwa wakisogea juu kupress ilikuwa bora sana


5. AGAIN. Unasifu mbinu za Minziro. Licha ya Simba kuja na Presha kubwa.. Geita waliendelea na mtego wao. Tazama Bao la Mpole lilivyokuwa. Wakati Simba wana 'Press' Geita wakachomoka kwenye mtego huo kwa Haraka na kufunga goli


6. Nimependa sana namna ambavyo Geita wanashambulia kwa idadi kubwa ya watu kwenye boksi la timu pinzani. Ni ishara ya kuandaliwa vyema kwenye uwanja wa mazoezi


7. Kipindi cha Pili Geita ni kama walichanganya zaidi. Wakafungulia busta zao. Wakauchukua mchezo na kumuacha Pablo akiwa na maswali mengi bila majibu


8. GEORGE Mpole🤛 HE IS ON FIRE! BAO LA 14 kwenye orodha ya wafungaji Bora. Mikimbio yake namna anavyonusa harufu za hatari, hahitaji nafasi nyingi akufunge, Muunganiko wake na Lyanga ni bora sana.


8. YUSUF KAGOMA na KEVIN NASHON leo walivuja jasho na kuwapa kazi ngumu Lwanga na Kanoute pale kati namna walivyokuwa wanapora mipira na kupiga basi ni kwa ubora mkubwa sana


9. KIBU D.. CHINI YA PABLO AMEZIDI KUIMARIKA. Ni kama presha imeshuka kwenye mabega yake. Kama kuna kazi benchi la Ufundi la Simba wanastahili kupongezwa basi ni jinsi Kibu alivyotunzwa kisaikolojia


10: Kagere hakustahili kumaliza mchezo. Red Card ilikuwa stahiki yake. Manula kaumia.. Kapombe..Bocco .. Chama pia. Inataka moyo kuwa shabiki wa Simba nyakati hizi


Nb: Tofauti yao na Arsenal ni zile jezi za Vunja Bei tu😃

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger