5/24/2022

Diamond Platnumz Katika Mtego, Mama Dangote Ataka Mkwe Awe Aaliyah, Mwenyewe Kazama Kwa Zuchu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAMtangazaji wa Wasafi TV, Aaliyah.
Mama Dangote; ni mama wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz ambaye habari za ndani kabisa zinadai kwamba anamkubali kinoma mtangazaji wa Wasafi TV, Aaliyah awe mkwe wake.

Kwa muda sasa kumekuwa na madai mazito kwamba, Diamond au Mondi anatoka kimapenzi na msanii wake, Zuchu ambapo madai hayo yanasemekana kumgombanisha Zuchu na Aaliyah ambao awali walikuwa marafiki wa kupika na kupakua huku wakiishi pamoja.

Lakini tangu kumekuwa na tetesi za Zuchu kutoka kimapenzi na Diamond, basi ushosti wao umegeuka uadui.

Sasa; kinachoendelea ni kwamba kwa sasa Aaliyah anashinda na kupika na kupakua na nyumbani kwa Mama Dangote huku akionesha upendo kama wote kwa familia hiyo.Mama Dangote
Inadaiwa kuwa, kinachomfanya Aaliyah kuiganda familia hiyo ni baada ya Mama Dangote kumuahidi kwamba awe mvumilivu na kuwa na subira hadi pale Diamond atakapotangaza ndoa.

Kinachombeba Aaliyah ni kwamba anakubalika kwa Mama Dangote na dada wa Diamond, Esma Platnumz ambao kwa kawaida ndiyo huwa waamuzi wa mwisho juu ya ni mwanamke gani awe na kijana wao.

Hata hivyo, kwa upande wa Zuchu, watu wake wa karibu wanasema anachokifanya Aaliyah ni kumrusha roho Zuchu ambaye naye humuambii kitu kwa Diamond au Simba wa Tandale.


Inaelezwa kwamba, anachokifanya Zuchu ni kuendelea kumkoleza Diamond kwa mahaba tele na vijizawadi vya hapa na pale ili kumfanya asisikie la mtu kwake na mpaka sasa jamaa huyo amekaa kwenye kumi na nane zake.HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger