Muimbaji wa Destiny's Child, Kelly Rowland hatimaye amenyoosha maelezo kufuatia uvumi kwamba kundi hilo (Destiny's Child) lipo mbioni kuerejea kwaajili ya kufanya muziki mpya na tamasha lao la muziki.
Kupitia mahojiano na Entertainment Tonight, Kelly Rowland amesema "Tunampenda kila mtu sana ila nadhani jambo hili linastahili kuwa la kushtukiza zaidi, kila kitu kitapangwa ila mtashtukizwa tu, itakuwa surprise mzuri".
Kundi hilo linaloundwa na mastaa watatu akiwemo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams ambao waliachana mwaka 2006 na kila mtu kufanya kazi peke yake. Ni ndoto ya muda mrefu kwa mashabiki wa kundi hilo kuona lina rejea.
Wimbo wao wa 'Survivor' ulitingisha sana na kuwapa heshima kubwa.
✍️: @omaryramsey
#SNSEnt
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
________________________________
Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE
0 Blogger:
Post a Comment