5/04/2022

Rais Samia Kuwataja Waliochangia Pesa Kutengeneza Filamu ya Royal Tour


Rais Samia Suluhu Hassan amesema wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour jijini Dar es Salaam Mei 8 mwaka huu watawataja watu/taasisi zote zilizochangia fedha iliyotumia kutayarisha filamu hiyo inayoangazia fursa za utalii na uwekezaji nchini.

Akifanya mahojiano na Azam TV, Rais amesema katika uzinduzi wa Arusha waliwashukuru watu hao kwa ujumla, lakini Dar es Salaam watamtaja mmoja mmoja.

"Zile bilioni 7 sikuchukua serikalini, nilichangisha kwa wafanyabiashara ambapo watafaidika na yatakayotokana na ile filamu... Tutakapokuwa Dar es Salaam tutamtaja kila mmoja aliyechangia," amesema.

Aidha, amesema kiwango hicho cha fedha kinaweza kuonekana na kikubwa, lakini kuzingatia ubora wa filamu hiyo yenye viwango vya Hollywood, na matokeo yake itakayoleta kwenye utalii, biashara na uwekezaji, yatakuwa ni makubwa huku akisisitiza kwamba "ninajua nilichokifanya."

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger