5/27/2022

Video ya wimbo "Sukari" ya msanii Zuchu Yafikisha Watazamaji Milioni 72

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Video ya wimbo "Sukari" ya msanii @officialzuchu kutoka lebo ya WCB, imefikisha zaidi ya watazamaji Milioni 72 katika mtandao wa youtube kwa mwaka mmoja na miezi mitatu. Ilipandishwa youtube Januari 2021.

Zuchu ambaye ana miaka miwili tangu atambulishwe rasmi na lebo yake, anakuwa msanii wa kwanza wa Tanzania (solo) kufikisha idadi hiyo kubwa ya watazamaji. Pia amefikisha views zaidi ya milioni 323 YouTube na kuwa msanii kike namba tano kusini mwa Jangwa la Sahara kufanya hivyo.

Wanaomtangulia ni Sinach (views milioni 654), Yemi Alade (milioni 633), Tiwa Savage (milioni 374) na Ada Ehi (milioni 323.7), wote hawa ni kutokea Nigeria.

Ikumbukwe, @officialzuchu amekuwepo kwenye chati za YouTube Music nchini Tanzania kwa wiki 109 na ndiye msanii wa kike Bongo aliyekaa kwenye chati hizo kwa muda mrefu zaidi.

✍️: @omaryramsey

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger