6/10/2022

Diamond Platnumz na Zari Hassan Wakutana Nairobi Kenya

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Supastaa Diamond Platnumz amewasili leo jijini Nairobi nchini Kenya kwa mujibu wa chapisho lake kupitia Insta story.

Bila kuweka wazi zaidi kuhusu safari yake hiyo ya mjini Nairobi, Diamond ame-share kipande kidogo cha video akiwa ndani ya ukumbi wa CIP Lounge katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dare es salaam. “Nairobi Usiku wa leo!”. Yalisomeka maneno ya Diamond.

Diamond amewasili nchini Kenya muda mmoja na mzazi mwenzie Zarina Hassan.

Kwa upande wa Diamond bado haijawekwa wazi ni kipi kilichompeleka nchini humo japo kwa upande wa Zari yeye anatazamiwa kuandaa sherehe yake ya kila mwaka ya All White Party jijini Nairobi leo Juni 9.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Brooklyn City alitaja kuwa hafla hiyo ya hadhi ya juu itafanyika XS Millionaires Club na mashabiki wake wote wamealikwa kuhudhuria.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger