6/16/2022

Diamond Platnumz ni Kama Maji...Dulla Makabila Achutama na Kumpigia Magoti Mond " Wasafi ilinifanya Niwe Brand"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


dullamakabila

 


Dulla Makabila Ameandika haya:

"Diamondplatnumz Bigi ni ukweli usiopingika kwamba nimepoteza mtu muhimu sana kwenye career yangu ambae ni wewe na vita pekee ya kuomba radhi haiendewi na silaha mikono yangu ipo nyuma naomba unisamehe sana kaka kwa yote yaliyotokea nikisema leo nisielezee hisia zangu na jinsi navyojiskia baada ya kuwa mbali na wewe na familia nzima ya #wasafi kisa eti labda nitaonekana najishusha au nna shobo au sijiamini na kipaji changu nitakuwa najidanganya mwenyewe maana ni ukweli usipingika kwamba dullamakabila alikuwa star kabda ya kuwa na wasafi na ni ukweli usiopingika kwamba WASAFI Ndio Walifanya dullamakabila awe brand na kutofautiana na wasanii wenzie wa singeli naweza nisiwe sehemu ya historia ya mafanikio yako ila naamini wewe una nafasi kubwa kwenye maisha yangu sihitaji kuelezea ni mangapi mazuri uliyafanya kwangu maana yananitafuta ndani kwa ndani 😔 na wala sitaki kumlaumu mtu wala kusema fulani ndo kaniponza ila uongo hautaenda mbali kama ukweli kuwa kuna mahali nimeteleza nahitaji kusamehewa BIGI Naiomba nafasi hii tena ya kuwa miongoni mwa wale wanaoamini katika wewe na naahidi kuwa dulla mpya ambae atopelekeshwa tena na miluzi mingi naomba unisamehe bro na wasafi nzima kwa ujumla naomba mnisamehe sana pia nyinyi ni Famila yangu"


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger