Ticker

6/recent/ticker-posts

Geita: Mpole ruksa kuondoka
MWANZA. LICHA ya taarifa kueleza kuwa tayari Geita Gold wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja kinara wao wa mabao, George Mpole mabosi wa timu hiyo wamesema hawana roho mbaya na watamfungulia milango atakapohitaji kuondoka.

Mpole alisaini mkataba wa mwaka mmoja Agosti 16, 2021 akitokea Polisi Tanzania ana mabao 16 na asisti tatu sawa na Fiston Mayele wa Yanga ambaye anamzidi Mpole kwa asisti tano.

Nyota huyo anahusishwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao huku taarifa zikisema amemalizana na mabosi wa Msimbazi baada ya kutoka kwenye mechi za timu ya taifa Juni 8, mwaka huu.

Akizungumzia uwezekano wa Mpole kuondoka, Katibu wa Bodi ya klabu hiyo, Zahara Michuzi alisema hadi sasa hakuna timu iliyowasilisha barua ya kumhitaji lakini milango iko wazi kama atahitaji kuondoka.


 
“Tumefanya naye mazungumzo hadi sasa hatujapata barua rasmi ya kusema timu gani inamtaka lakini kama mapenzi yake yatatamani kwenda nje ya Geita Gold milango iko wazi, kuondoka kwa mmoja ndiyo kuja kwa wengine wengi riziki ndiyo iko hivyo.

“Kwahiyo kama atapenda kuondoka Mpole mmoja tutaongeza Mpole watatu, tulishaboresha maslahi ya wachezaji wetu na hata mikataba inayokuja tutakaa nao wote mezani kwa ajili ya maslahi ya jumla lazima tuyazingatie,” alisema.

Awali Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mathias Wandiba alisema; “Nafikiri suala la Mpole tujipe muda ni mchezaji anayehitaji mafanikio makubwa kwahiyo akipata mafanikio hayo anaweza akaenda, naamini kwa sasa focus yake kaweka kuhakikisha Geita Gold inamaliza katika nafasi nzuri.”


Mpole amekuwa gumzo kwa sasa kutokana na mashabiki wengi kufuatilia kasi yake ya kutupia huku wakitamani aibuke kinara apate mzuka zaidi wa kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa katika mashindano yaliyoko mbele yake kwani amekuwa chaguo la Kim Poulsen.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments