6/07/2022

Hii Ndio Sababu ya Kajala Masanja Kuwa Meneja Konde Gang

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Hatimaye Lebo ya muziki ya Konde Music maarufu Konde Gang iliyochini ya msanii Harmonize imeweza kufunguka sababu ya kumteua Kajala Masanja kuwa Mkurugenzi Mtendaji (C.E.O) wao.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Meneja wa Harmonize, @choppa_tz amesema @kajalafrida ana uwelewa mkubwa kuhusu muziki na anajua soko linahitaji nini hasa.

"Ni kweli tumetangaza kama Kajala ni Meneja na Mkurugenzi pia, kuhusiana na majukumu yake yatakuwa ya kawaida 'as a manager' ni ku-manage shughuli zote za Konde Music Worldwide kuanzia kwa Harmonize mpaka wasanii wengine kama ilivyo sisi kwa ma-meneja wengine" - amesema Choppa.

"Kajala sio mgeni, yupo kwenye hii Industry kwa muda mrefu sana hata kama kwa upande wa movie lakini movie na mziki ni vitu vinavyoshabihiana. Ni vitu ambavyo anavijua, ana ique kubwa sana, anaelewa mziki na soko linataka nini na hakuna kitu kigeni kwake" aliongeza Choppa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger