6/07/2022

Mariah Carey Ameripotiwa Kufikishwa Mahakamani Kwa Kosa la Hatimiliki Kupitia Wimbo wake

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwimbaji nyota wa muziki toka Marekani, Mariah Carey ameripotiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la hatimiliki kupitia wimbo wake "All I want for Christmas is you".


Kwa mujibu wa nyaraka zilizodakwa na TMZ, mwimbaji Andy Stone anasema aliandika wimbo wa "All I want for Christmas is you" mapema mwaka 1989. Anadai kuwa wimbo huo ulipata mafanikio makubwa kwa kuingia kwenye charts za billboard 1993, huku wimbo wa Mariah Carey ulitoka 1994 ukiwa unapatikana kwenye album yake iliyoitwa "Merry Christmas".


Hata hivyo Andy Stone anadai kuwa Mariah na team yake hawakuwahi kuomba kibali cha kutumia jina la wimbo huo hivyo anataka alipwe kiasi cha $20 Milioni ambazo ni takribani Tsh Bilioni 46.5 kama fidia.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger