Manara afichua SIRI ya usajili Young Africans

 


Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara, ametamba klabu hiyo itafanya usajili mkubwa utakaozingatia ripoti ya Benchi la Ufundi.

Young Africans imepanga kufanya usajili huo, huku ikiwa klabu pekee msimu huu 2021/22, iliyoonyesha kuwa na kikosi imara ambacho hakijapoteza mchezo hata mmoja wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Manara amesema klabu hiyo ina malengo makubwa kuelekea msimu ujao, hasa ikizingatiwa itashiriki Michuano mikubwa Barani Afrika, hivyo watahakikisha wanapata wachezaji wenye hadhi ya juu.

Amesema pamoja na kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kupambana msimu huu, bado Uongozi unaamini ripoti ya Kocha Mohamed Nabi itatoa mapendekezo ya usajili ambayo lazima yatafanyiwa kazi kwa asilimia 100.

“Tuna malengo makubwa na tunajua wapi ambapo tulishindwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa tutasajili wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa ili kuleta ushindani kimataifa,” amesema Manara.

Hadi sasa Tetesi zinaeleza kuwa Young Afrcans huenda ikawaacha wachezaji zaidi ya 10 mwishoni mwa msimu huu, huku ikiwa tayari imeshaachana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake, pia alihusishwa na utovu wa nidhamu wakati timu ilipoweka Kambi jijini Mwanza kwa maandalizi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC”.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad