6/21/2022

Mbunge ahoji misafara ya viongozi kusababisha foleni barabarani

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA
Dodoma. Mbunge wa Kyela, Ally Jumbe ameeleza  kero wanayoipata watu wakati wakisubiri misafara ya viongozi kupita kwenye barabara mbalimbali nchini.

Akichangia bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2022/23 leo Jumatatu Juni 20,2022, Jumbe amesema usalama wa viongozi nchini ni  muhimu lakini usalama huo kuna maeneo unawakwaza Watanzania.

“Utakuta kiongozi wetu anasafiri ama anapita sehemu saa tano  asubuhi lakini magari yanaanza kufungiwa kupita kuanzia saa 12 asubuhi."

"Spika hili halikubaliki katika teknolojia ya sasa hivi ni nani amewahi kufanya utafiti wa madhara yanayotokea? Mfano mtu alikuwa anaenda mahakamani, halafu akafungiwa mnajua ni watu wangapi  wameshindwa kufika mahakamani,” amehoji.


 
Ameomba watumie njia rahisi ambayo viongozi wanaweza kusafiri hata kwa  helkopta akibainisha kuwa kwa sasa Tehama inafika  maeneo mbalimbali na kuhoji kwanini hazitolewi taarifa mapema za barabara zinazotumika wakati viongozi wanapita.

“Kama unawahi sehemu uwahi kuondoka. Katika uchumi huu tunaokwenda muda ni muhimu sana tusichezee muda huu,” amesema.

Amesema juzi walikaa kwenye mzunguko (hakuutaja) kwa zaidi ya dakika 40 wakati wanakwenda bungeni lakini baada ya muda huo waliruhusiwa kuendelea na safari bila kiongozi kupita.


“Hii sio nchi ya kujenga uchumi wa blablaa, tujengee uchumi uliokamilika,” amesema.


 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger