6/13/2022

Msanii wa Nigeria Burna Boy Akumbwa na Msala Mzito wa Kujaribu Kuua

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


BURNA BOY; ni staa mkubwa wa muziki wa Nigeria anayeshikilia Tuzo ya Grammy ambaye ameingia kwenye msala mzito mno wa mauaji.


Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi wa Lagos nchini Nigeria, wanawashikilia maofisa watano wa Polisi wenye ukaribu na Burna Boy kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili kwenye Klabu ya Cubana usiku wa Juni 8, mwaka huu.


Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Polisi hao wanaomlinda Burna Boy walifika kwenye klabu hiyo na staa huyo ambaye alikwenda moja kwa moja kwenye sehemu ya VIP akiwa na wanawake watatu.


Lakini wakiwa wanaendelea na starehe, Burna Boy alimuona mwanamke mwingine mzuri mno ambapo bila kujua ni mke wa mtu, Polisi mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Ibrahim alimfuata mwanamke huyo na kumuambia Burna Boy anamtaka aungane naye kwenye kula bata.


Kufuatia hilo, mume wa mwanamke huyo alimwambia Polisi huyo kwamba mwanamke huyo hawezi kuungana na Burna Boy na kwamba staa huyo alimkosea heshima.


Hapo ndipo kulipotokea vurugu kubwa ambapo mmoja wa maofisa hao wa Polisi alimpiga risasi ya kwenye paja mume wa mwanamke huyo na mtu mwingine alipigwa risasi kichwani na wanaendelea na matibabu baada ya kutolewa risasi mwilini.


Inaelezwa kwamba wakati risasi zikipigwa, Burna Boy alikuwa akiamrisha wapigwe risasi huku akifurahia.


Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, Burna Boy anadaiwa kutorokea nchini Hispania ambapo anasakwa ili akamatwe kwa msala huo huku Polisi hao wawili wakiwa nyuma ya nondo za mahabusu.


Cc; @sifaelpau

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger