Ticker

6/recent/ticker-posts

Fiston Mayele Aipa Mbinu Taifa StarsMshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ameizungumzia mechi ya Tanzania na Somalia kwa kuitahadharisha Stars kuwa makini kutokana na ukweli wapinzani wao sio timu ya kubezwa.

“Somalia nimecheza nao nikiwa na Yanga katika mechi ya kirafiki na kutoka nao sare ya 1-1, ni timu nzuri, ni lazima Stars iwe makini hata kama bado naipa nafasi kubwa ya kushinda mechi zote mbili za kufuzu Chan,” alisema Mayele na kuwataja Feisal Salum, Salum Abubakar na Bakar Mwamnyeto kuwa wataibeba nchi yao kama walivyoibeba Yanga msimu uliopita.

Stars itaivaa Somalia katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Chan mchezo wa kwanza ukipigwa Julai 23 kabla ya kurudiana tena wiki moja baadaye, michezo yote ikipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments