Mwimbaji H.Baba afunguka namna alivyochukizwa na kitendo cha aliyekuwa mkewe Flora Mvungi kuandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa instagram siku chache nyuma.
"Unajiita baba halafu wanao wanalelewa ukweni. Pambana wewe! Baba sio jina la ubatizo mfyuuu".... ilisomeka sehemu ya ujumbe huo mrefu wa Flora kupitia ukurasa wake ambao ni wazi kuwa ulienda kwa mzazi mwenzie H.Baba waliyepata nae watoto wawili.
Akizungumza kwenye Chill na Sky, H.Baba amekiita kitendo hicho ni ukosefu wa heshima na nia ya Flora ni kutaka kumkomoa. H.Baba pia amebainisha kuwa hajawai kumpa talaka Flora Mvungi, licha ya sasa kuwa ni walezi tu kwa watoto wao.
Kadhalika na hilo, H.Baba amewachana baadhi ya wasanii wakike Bongo wenye tabia za kuharibu ndoa/mahusiano ya watu ambao ndio walioharibu mahusiano yake na Flora.
0 Comments