Mayele, Inonga, Bangala kuwania uchezaji bora leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




SHEREHE za Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), msimu wa 2021/22, zinafanyika leo, Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimegawanyika katika makundi mbalimbali, zikiwemo Tuzo za Kikanuni za mashindano, Tuzo Binafsi za wachezaji na waamuzi, Tuzo za Heshima na Tuzo za Kiutawala zikihusisha wasimamizi wa mpira wa miguu na wadau wengine waliotoa mchango wao kwa mchezo huo.

Mbali na tuzo za kawaida zinazohusiana na mashindano kwa maana ya bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na wa nne, kutakuwa na tuzo binafsi 57, zikiwemo zile zinazotolewa kwa mtu zaidi ya mmoja, mfano Seti Bora ya Waamuzi, Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya Wanawake na Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya NBC.

Kwa mara ya kwanza kutakuwa na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Championship na wa First League.


 
Tuzo ya mchezaji Bora Ligi Kuu ya NBC (NBC PL) inawaniwa na Henock Inonga – Simba SC, Yanick Bangala – Young Africans na Fiston Mayele – Young Africans.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad