Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwimbaji Zuchu Amefunguka Kuhusu Collabo na Nandy na Diamond Platnumz

 


Zuchu amefunguka kuhusu kufanya kazi na Nandy pamoja na Diamond Platnumz ambaye wamefanya wote takribani nyimbo tatu ambazo tayari zimetoka.


Akizungumza kwenye kipindi cha Mgahawa cha Wasafi FM, @officialzuchu amesema muda ukifika atafanya kazi na Nandy.


"Mimi na nandy tunajuana muda mrefu, tangu anatoka namuona. Muda ukifika nitafanya nae kazi" amesema Zuchu akijibu swali kuhusu kwanini hajafanya collabo na Nandy hadi hii leo.


Aidha, pia ameabainisha kwamba amejijengea kuwa yeye kwanza, haipi kipaumbele collabo na kusema hata katika album yake atakuwa yeye tu.


Sanjali na hilo, pia ameeleza kuhusu wimbo wake mpya "Fire" akisema hapo awali aliimba na Diamond lakini baadae aliitoa verse yake kwa kuwa walishaimba wote kwenye wimbo Mtasubiri ambao una miezi mitatu tangu utoke.


"Fire ni wimbo niliotakiwa niimbe na Diamond Platnumz na verse ya pili aliimba yeye. Kwa hiyo niliiondoa kwa sababu tulishaimba wote," ameeleza Zuchu.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments