Saa zahesabika hukumu kina Mdee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MAHAKAMA Kuu Masijala Kuu imeshindwa kutoa uamuzi wa maombi ya Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, na wenzake 18 ya kibali cha kuwasilisha mapitio ya kimahakama wakipinga kuvuliwa uanachama wa CHADEMA, kwa kuwa uamuzi huo haujakamilika.
Saa zahesabika hukumu kina Mdee


Katika taarifa yake jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Elimo Masawe, alisema uamuzi haujakamilika na hivyo shauri hilo limeahirishwa hadi Ijumaa, yaani kesho saa sita mchana.Uamuzi huo ulitarajiwa kutolewa na Jaji Mustapha Ismail ambapo waleta maombi (Mdee na wenzake) waliwasilisha hoja tano za kisheria kuishawishi mahakama itoe kibali hicho kwa kuwa maombi hayo waliyafungua ndani ya muda.Wakati wakiwasilisha hoja zao, Wakili wa Mdee na wenzake, Ipilinga Panya, alidai wamewasilisha ombi hilo wakiwa na hoja tano ikiwamo ya kwamba wamefungua maombi hayo ndani ya muda wa kisheria.Alidai hoja nyingine ni kuonyesha kuna jambo linalobishaniwa, kuonyesha maslahi ya waleta maombi, CHADEMA ni chombo cha umma na kama walitafuta haki zao ndani ya chama hicho.Wakili Panya alidai maombi hayo yamefunguliwa kwa wakati kwa kuwa yalitakiwa yaombwe ndani ya miezi sita tangu kutolewa kwa uamuzi unaolalamikiwa na hivyo Mdee na wenzake wamefungua maombi  yao ndani ya muda.Alidai waleta maombi wote ni wabunge wa viti maalum walioteuliwa na Bodi ya Chama hicho mwaka 2020-2025, hivyo uamuzi wa kuwafukuza uanachama bila kufuata utaratibu wa kuwasikiliza, unagusa maslahi yao binafsi.Wakili Panya alidai Mdee na wenzake wana maslahi mapana katika jambo hilo, wameathirika na uamuzi wa bodi hiyo kupitia uamuzi  wa Baraza Kuu la Chama hicho wa Mei 11, 2022 uliowafukuza uanachama.Wakili Peter Kibatala katika kujibu hoja hizo, alidai hawabishi hoja kwamba Mdee na wenzake wana maslahi mapana ila kigezo cha mgogoro hakiangaliwi juu, bali lazima kuwapo ushahidi mahakamani chini ya kiapo ili mahakama ichunguze  na hawajauwasilisha.Alidai hawabishi kwamba waleta maombi kwenda mahakamani,  lakini njia waliyotumia ilikuwa si sahihi, kwa kuwa walichelewesha haki zao kwa kuiomba mahakama kwa njia ya mapitio.Wakili Kibatala alidai watu  28 hawawezi kubadili uamuzi wa wajumbe 437,  waleta maombi walikuwa wanaijua Katiba ya Chadema na kwamba wajumbe wa Kamati Kuu wanaingia katika Baraza Kuu, hivyo haikuwahi kuleta shida, haiwezi kuwa hoja ya msingi.Kibatala alidai kwamba CHADEMA siyo chama cha umma na hakifanyi kazi za umma kama ilivyoelezwa na waleta maombi.Mdee na wenzake walifungua kesi hiyo dhidi ya Baraza la Wadhamini la CHADEMA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad