Ticker

6/recent/ticker-posts

Watu watano wafariki, 48 wajeruhiwa ajali ya basi
Watu watano wafariki, 48 wajeruhiwa ajali ya basi
WATU watano wamekufa na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Sasebosa lililokuwa likitoka mkoani Mbeya kwenda Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alisema ajali hiyo ilitokea saa 11 jioni katika Kijiji cha Mabangwe wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Alisema chanzo cha ajali ni kupasuka tairi la mbele kushoto na kwamba lilikuwa na mwendo wa kasi uliosababisha dereva kushindwa kulimudu na hatimaye likaanguka.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sikonge, Dk Peter Songoro, baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wametibiwa na kuruhusiwa na wengine wanaendelea na matibabu wakiwamo sita waliopelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete ambayo ni ya mkoa.


 
Ajali hiyo imetokea ikiwa ni takribani wiki moja tangu ilipotokea ajali nyingine, Juni 25 mkoani Tabora ambayo askari watatu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na raia watatu walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na lori.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments