Diamond Platnumz Kuanzisha Shirika la Ndege

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Supastaa @diamondplatnumz hataki kuishia katika umiliki wa ndege yake binafsi (private jet) na Helikopta (Helicopter) tu alizonunua, anataka awe na Shirika kabisa la Usafiri wa Anga.


Boss huyo wa WCB amefunguka hayo jana Alhamisi, Agosti 11 kwenye kipindi cha #TheTouchDown cha radio ya nchini Afrika Kusini iitwayo Metro FM ambapo ameeleza kwa mara ya kwanza mpango wake huo wa kuanzisha shirika lake la ndege ambalo amelitaja linaitwa WASAFI AIRLINE.


Aidha, Diamond hajaeleza kwa kina kuhusu mikakati yake hasa juu ya shirika hilo, lakini ameweka wazi kwa mara ya kwanza kwamba anaelekea kuanzisha shirika hilo.


"Nilianza kujiwekeza katika muziki, nikaanzisha lebo, nikafungua vituo vya habari (TV na Radio), nikaanzisha Kampuni ya michezo ya kubashiri (Wasafi Bet) na sasa nipo naelekea kufungua shirika la ndege." - ameeleza @diamondplatnumz ambaye amekuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa nchini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad