Rais Samia: Kenya imeonyesha Ukomavu wa Demokrasia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kuonyesha ukomavu wa demokrasia huku akisema wametoa zawadi pekee ya amani wakati wa uchaguzi kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Rais Samia ameeleza hayo leo Septemba 13, 2022 jijini Nairobi wakati wa sherehe za kuapishwa kwa William Ruto kuwa Rais, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 9 na kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Rais Samia amesema wananchi wa Kenya wameonyesha ukomavu wa demokrasia Afrika Mashariki na kusisitiza kwamba sasa uchaguzi umekwisha, wasimame imara kuijenga nchi yao ya Kenya.

Rais mteule wa Kenya, William Ruto akizungumza na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ofisini kwake, Karen, jijini Nairobi nchini Kenya

“Ndugu zangu Wakenya, tunawapongeza nyinyi kwa kuonyesha ukomavu wa demokrasia na kumaliza uchaguzi salama na leo tuko hapa pamoja kama Wakenya na wa-East Afrika tukishangilia uapisho wa Rais wetu mpya.


“Nataka niwaambie ndugu zetu Wakenya, kama kuna zawadi mliyoitoa kwa Afrika Mashariki mwaka huu, ni zawadi ya amani mliyoiweka katika uchaguzi. Tunawashukuru sana kwa zawadi hiyo muhimu,” amesema Rais Samia.

________________

KISASI CHA USALITI PENZINI !!!,usipoipenda simulizi hii dai Mb na pesa zako,licha ya kuenjoy mahaba ndani yake kuna kitu cha kujifunza mwishoni Bofya Hapa kusoma Sehem ya 1 bure,sehem iliyobaki tsh 2000 kwa mtandao wowote.

Tembelea www.makapedia.com kwa stori mpya kila tarehe moja.


JE UNATAKA BIASHARA YAKO IWE YA UHAKIKA MIAKA YOTE YAJUE HAYA? usikose kitabu hiki Bofya Hapa kusoma sehem ya 1 bure sehem ya 2 tsh 2000 tu 

ndani ya www.makapedia.com

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad