Wema Sepetu Atamba Kuwazidi Wanawake Bongo Kwa Followers Instagram


Supastaa Wema Sepetu ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006 ni habari nyingine, nyota huyo ambaye ana miaka zaidi 16 kwenye gemu ni miongoni mwa mastaa wa kike nchini waliyodumu kwenye kiwanda cha burudani kwa muda mrefu akiwa bado anaendelea kusumbua.

Good news kwa mashabiki wa @wemasepetu ni kwamba amefanikiwa kufikisha followers Milioni 10 kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kufanya hivyo.

Aidha, Wema amebainisha kwamba hataki kushindanishwa na yeyote yule kwani naye hajawahi kushindana na mtu. Ameeleza kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuongoza kuwa na followers wengi kwa wanawake nchini.

"Nabaki kuwa wa kike wa kwanza Tanzania kufikisha 10M, basi naombeni kuanzia sasa, msinishindanishe na mtu jamani. Atakaefuata na kunizidi isiwe battle basi wapenzi wangu. Tumefikisha 10M bila nguvu yoyote, nitumie tu nafasi hii kusema ASANTENI na NAWAPENDA. ❤️๐Ÿ’š❤️." - @wemasepetu

Fahamu, anayemfuata Wema ama kumkaribia ni mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye ana followers Milioni 9.9, kisha Shilole mwenye followers Milioni 9.4


______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ๋†€๋‹ค ๋ฐ”์นด๋ผ ์ง€๊ธˆ ์˜จ๋ผ์ธ์œผ๋กœ ๋ผ์ด๋ธŒํ•˜๊ณ  ๋†€๋ผ์šด ๋ณด๋„ˆ์Šค๋ฅผ ๋ฐ›์œผ์„ธ์š”

    ReplyDelete

Below Post Ad