Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Yasogeza Mbele Mechi za Yanga, Simba na Azam FC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Wachezaji wa Yanga Feisal Salum na Stephen Aziz Ki wakishangilia bao dhidi ya Azam FC

BODI ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imetangaza kusogeza mbele baadhi ya michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo inahusisha vilabu vinavyoshiriki katika michuano ya Ligi ya Mbaingwa Barani Afrika ikiwemo Yanga, Simba na Azam FC.


Mshambuliaji wa Simba raia wa Zambia Mose Phiri

Mchezo wa Klabu ya Yanga dhidi ya Namungo FC, ambao ulipangwa kuchezwa tarehe 13 Oktoba, 2022 kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi umeahirishwa hadi pale utakapotangazwa tena.

 

Vivyo hivyo kwa michezo kati ya Singida Big Stars dhidi ya Simba SC na mchezo mwingine kati ya Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji.


Azam FC

Bodi ya Ligi imefanya maamuzi hayo ili kuzipatia klabu hizo muda mzuri wa maandalizi, kusafiri na kushindana kikamilifu kuelekea kwenye michezo wa marudiano katika hatua ya mtoano kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad