Fred Vunja Beo Afunguka "Mafanikio Hayakufuati Bali Yanafuatwa...Acha Lift Panda Ngazi"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAKutoka kwenye ukurasa wa instagram wa @fred_vunjabei Ameandika...

"ACHA LIFT PANDA NGAZI;

Mara nyingi MAFANIKIO hayakufuati ni vyema ukayafuata, unasubiri lift muda mrefu kumbe kuna watu wameizuia wanapiga picha, kuna mwanazuoni alisema wakifunga mlango jaribu dirisha. Ni vyema ukapanda ngazi hata kama ni vigumu “Nothing worthy having comes easy”

Watu wengi huamini mafanikio yao yapo kwa mtu fulani unasubiri miaka mingi huzioni dalili njema, wengine huamini kupitia biashara fulani na ni muda haikupi matunda, wengine huamini hawezi kujiajiri anang’ang’ania ajira ambayo hamlipi miaka yote, unachelewa kufanya maamuzi. Panda ngazi acha kusubiri lift.

Subira yavuta heri lakini ngoja ngoja yaumiza matumbo jiwekee ukomo wa kusubiri, tafuta njia nyingine ya kupita ili ufikie mafanikio yako kwa haraka. Kuna uwezekano njia aliyokupangia Mungu sio hiyo unayolazimishia kupita. Get out of the box!!

Mimi binafsi ajira haikuwa njia yangu niliamua kubadili na kuacha kazi serikalini japokuwa ilikuwa ngumu nili- take risk, sio RISK tu bali calculated one, “the higher the RISK the higher the RETURN”

Fred Vunjabei (2022)"

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad