Simba Hali Mbaya...Yadondosha Pointi Mbili Mbeya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPAMbeya. Dakika 90 za mechi ya Mbeya City imemalizika kwa timu hizo kutoa sare ya bao 1-1 huku mabao ya Mzamiru Yassin (Simba) na Tariq Seif yakitosha kumaliza mtanange huo.

Hizi ni dondoo za mechi hiyo;

Bao la Mzamiru Yassin alilofunga linakuwa la pili kwake msimu huu na kufikisha mabao 30 kwa Simba kuihenyesha Mbeya City waliofikisha mabao saba .

Katika dakika 90 za mchezo huo Simba ilipata kona saba kwa mbili huku mchezaji wa Mbeya City, Hassan Mohamoud akioneshwa kadi ya njano dakika ya 38 baada ya kumchezea rafu Moses Phiri.

Simba inashindwa kulipa kisasi kwani msimu uliopita ikicheza uwanjani hapo Sokoine ililala bao 1-0 likifungwa na Paul Nonga, huku wao wakikosa penalti kupitia kwa nyota wake wa zamani, Chris Mugalu aliyegongesha mpira kwenye nguzo na leo inaondoka na pointi moja.


Bao la Seif linafika la tano kwake hadi sasa huku Awadh Juma akifikisha asisti ya tatu kwa Mbeya City na kuendelea kutengeneza uhusiano mzuri baina yake na Straika huyo sambamba na Sabilo.

Simba imewapumzisha Bocco, Okrah na Phiri na kuwaingiza Kibu Denis, Kyombo na Sakho. huku City wakimtoa Ngy'ondya na kumwingiza Gasper Mwaipasi.

Hii inakuwa sare ya pili kwa timu hizo katika michezo 15 waliyocheza huku ikiwa ya nne tena kwa Simba msimu huu baada ya kulazimishana bao 1-1 na Singida Big Stars ikiwa ugenini, Yanga 1-1, KMC 2-2.


Simba imefikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu huku Mbeya City ikiwa nafasi ya sita na pointi 19.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad