Ticker

6/recent/ticker-posts

Watano wafariki shambulio la risasi ukumbini

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAPolisi wa Colorado Springs, wamesema takriban watu Watano wamekufa, na wengine 25 kujeruhiwa katika tukio la mwanamume mmoja aliyeingia ndani ya klabu ya usiku akiwa na bunduki ndefu na kuanza kuwafyatulia risasi wateja na wafanyikazi wakati wa hafla ya Drag Divas iliyoandaliwa na uongozi wa eneo hilo.

Mkuu wa Polisi, Andrian Vasquez amesema mshambuliaji huyo, Anderson Lee Aldrich (22), mkazi wa Colorado Springs alikuwa na bunduki mbili zilizopatikana katika eneo la tukio, lakini haijabainika ikiwa alitumia silaha zote kutekeleza mauaji hayo ndani ya ukumbi huo wa LGBTQ Business Club Q uliopo Colorado Springs.


Polisi wa Colorado Springs, wanasema takriban watu Watano wamekufa, na wengine 25 kujeruhiwa. Picha ya ABC News.
Hata hivyo, Polisi na vitengo vya zima moto wamesema walipokea simu kuitwa kwenye tukio majira ya asubuhi ya Novemba 20, 2022 kuwa kuna tukio la risasi zinazopigwa kwenye kilabu ambapo wafanyakazi wa dharura walifika na kukuta watu wawili wakiwa wamemdhibiti mshukiwa.

Mshukiwa huyo, kwa sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Colorado Spring ambapo Msemaji wa UCHEalth anasema vituo vyao vinatibu watu 10 kutokana na shambulio hili, lakini haviwezi kutoa maelezo mahususi kwa wakati huu.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments