Ticker

6/recent/ticker-posts

Familia ya Mtanzania aliyefia Russia waiangukia Serikali

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPADar es Salaam. Wakati kukiwa na taarifa kuwa Mtanzania aliyefia nchini Russia, Nemes Tarimo, alikuwa amejiunga na vikosi vya jeshi la nchi hiyo vinavyopambana na majeshi ya Ukraine, familia yake imeiomba Serikali kueleza undani wa kifo hicho.

Nemes aliyekuwa akisoma nchini Russia anadaiwa kufariki Desemba 2022, huku baadhi ya video zilizosambaa mitandaoni zikionyesha Mtanzania huyo akipewa heshima za kijeshi.
Mwananchi limefika nyumbani kwa familia ya Nemes, Mbezi kwa Msuguri jijini hapa na kukuta wanandugu wakiwa wamekusanyika, wakisema wanasubiri taarifa ya Serikali.

“Sisi tunafahamu kuwa mdogo wetu alienda Russia kuanzia mwaka 2016 kwa ajili ya kusoma lakini baada ya kutangazwa kwa kifo chake ndipo tunapoona kuwa amefariki kama mwanajeshi,” amesema dada wa marehemu, Salome Kisale.

Amesema kuwa taarifa sababu za kifo cha mdogo wake zinazoendelea kwenye mitandao wao hawazifahamu.


Salome amesema awali walipokea taarifa za kifo cha Nemes Desemba16, 2022.


“Taarifa za kifo cha Nemes tumezipokea, lakini hatukutaka kuzisema kwanza kwa sababu tulitaka kujua kama ni kweli.

“Ila ilipofika Januari, 2023 ndipo tulipo thibitisha kuwa amefariki lakini chanzo cha kifo bado hatujakifahamu,” amesema.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments