Harmonize Sukari Ya Wasanii Wa Kike Atakayemshirikisha Kwenye Wimbo Wake…

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


MSANII wa Bongo, Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize au Harmo ana nyota kwa wasanii wa kike.


Inaelezwa kwamba msanii yeyote wa kike atakayemshirikisha Harmonize katika ngoma yake basi wimbo huo hutoboa.


Imani hiyo imesababisha Harmonize kufanya kazi nyingi na wasanii wa kike Bongo, kwa kipindi cha miaka mwili iliyopita.


Hawa ni baadhi ya wanamuziki wa kike waliowahi kufanya kazi na Harmo ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Lebo ya Muziki ya Konde Worldwide na nyimbo zao kubamba sokoni.




ANJELLA

Wimbo wake wa ‘Kioo’ aliofanya na Harmo miezi saba iliyopita ulifanya vizuri mwaka jana 2022 na kufikisha watazamaji YouTube zaidi ya milioni sita.


Ngoma ingie ni ‘Toroka’ ambayo ipo katika miondoko ya Amapiano nao ulikuwa tishio.


Anjella alipojiunga Konde mapema tu aliachia wimbo uitwao ‘Kama’ hiyo ilikuwa  Aprili 11, 2021 ukawa wimbo wake wa kwanza kumshirikisha Harmonize.


Hata hivyo, kabla ya kutambulishwa kuwa msanii wa Konde Music tayari Harmonize alikuwa amemshirikisha Anjella kwenye wimbo ‘All Night’ uliotoka Februari 16, 2021.


Baadaye Harmonize akamshirikisha tena kwenye ngoma ‘What Do You Miss’ toka kwenye Albamu yake ya pili, High School iliyotoka Novemba 5, 2021.


JANE MUSSO


Msanii huyu ingawa alikuwa maarufu zamani kwa wimbo wake wa Omoyo lakini nyota yake ilizima.


Ni kama alizinduka usingizini na kuamua kumshikisha Harmonize kwenye Remix ya wimbo huo na kujikuta akirudi tena sokoni kama msanii mpyaaa!


Ngoma hii ipo mtandao wa YouTube kwa miezi 10 tu na tayari umetazamwa zaidi ya mara 90,000.


QUEEN DARLEEN


Ndiye First Lady wa Wasafi Classic Baby (WCB), alisainiwa mwaka 2017 baada ya Harmonize, Rayvanny na Rich Mavoko kuingizwa kundini.


Queen hii ilikuwa ni lebo ya pili kusaini baada ya G Records alipofanya na wasanii kama Alikiba na wengine.


Juni 2019 alimshirikisha Harmonize katika wimbo uitwao ‘Mbali’ uliofanya vizuri, hadi sasa video yake imetazamwa zaidi ya mara milioni 9.2 katika mtandao wa YouTube.


NANDY


Juni 2020 Nandy alimpa shavu Harmonize katika wimbo wake ‘Acha Lizame’ nao uliofanya vizuri na kutazamwa zaidi ya mara milioni kumi, ni moja ya kolabo za mwanzo kubwa kwa Harmonize kufanya baada ya kutoka WCB.


MAUA SAMA


Maua Sama alimshirikisha Harmonize katika wimbo wake, ‘Niteke Remix’ uliotoka Julai 2020 na kufanya ambao ulibamba na kutazamwa Youtube zaidi ya mara laki tano na nusu.


ABIGAIL CHAMS

Abigail Chams ameachia ngoma ‘Closer’ inayofanya vizuri sasa akimshirikisha Harmonize. Ndani ya miezi sita sasa umetazamwa zaidi ya mara laki sita.


Hata hivyo, licha ya muziki, Harmonize anasema kuwa amekuwa akiwindwa na wanawake wengi katika siku chache zilizopita baada ya taarifa za yeye kuachana na Kajala Masanja kusambaa.


Msanii huyo amekiri kuwa amechanganyikiwa kuhusu kinachofanya wanawake wengi wamfuate kila kona japo anadhani ni kutokana na ufanisi wake wa muziki na ‘mpunga’ alionao..


“Nimechanganyikiwa kuhusu hili… siku hizi wanawake wananipenda kuzidi ninavyoweza kuelezea, usikubali mtu akwambie. Labda ni kwa sababu ninaendelea kutajirika au ni kwa sababu ya nguvu zangu kimuziki.” Anasema Harmonize.


Stori na Na Elvan Stambuli

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad