Header Ads Widget


Mwigizaji Elba Kufungua Studio Kubwa ya Filamu Tanzania

Mwigizaji Elba Kufungua Studio Kubwa ya Filamu Tanzania

 Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus leo Jumatatu, Januari 30, 2023 amezungumza na kuwaelezea Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyofanya Davos nchini Uswizi tarehe 16-20 Januari, 2023.


Akiwa huko Rais Samia alikutana na Muigizaji maarufu wa Filamu Duniani kutoka Uingereza Idris Elba ambaye ni Balozi wa hisani wa Umoja wa Mataifa wa IFAD ambapo kukutana kwao na kufanya mazungumzo kumezaa matunda. Elba ameonesha nia ya kufungua studio kubwa ya Filamu Tanzania.


“Rais Samia alikutana na Idris Elba na Mkewe Sabrina ambao wao katika Uwekezaji wanataka kuja kuwekeza kuanzisha studio kwa ajili ya Filamu, kwa hiyo mazungumzo ndio kwanza yanaanza lakini yakifanikiwa ina maana hiyo studio itaweza kusaidia sio tu Tanzania lakini Afrika Mashariki na kati” - ameeleza Zuhura Yunus leo katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments