Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwigizaji Batuli Alia na Mke wa Dr Mwaka..."Anahitaji Usaidizi, Ndo Zimejaa Manyanyaso Mengi"

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Batuli mama wa watoto wawili ambaye alishaishi maisha ya ndoa hata kabla ya kuwa mwigizaji maarufu afunguka kwa uchungu katikati ya gogoro la kindoa baina ya Queen na Dr.Mwaka

"Tumezoea Kusubiri Mtu Afe Ndio Tutafute Cha Kuongea, Wanawake Wengi Tunaishi Na Wenza Wetu Ili Watu Watuone Tupo Kwenye Maisha Ya Ndoa Ila Ukweli Ni Kwamba Wengi Wetu Ni WATUMWA Na Tunaishi Aidha Kwa Kulea Watoto Wakue Au Siku Ziende Kifo Kifike Tuondoke Huo Ndio Ukweli Wa 100%" ameandika Batuli na kuendelea..

"Machozi, Maumivu, Mateso Na Unyanyasaji Ndio Vimejaa Kwenye Ndoa Nyingi Sana Na Akisimama Mwanamke Mmoja Kama Huyu Basi Anaonekana Hana Uvumilivu Na Kubezwa Juu Na Ukikaa Kimya Na Kukubali Haya Kifo Chako Ndio Kinakuja Kuongea, Mbaya Zaidi Akitokea Au Wakitokea Wanaume Kusimama Na Wewe Watachafuliwa Kwa Hali Na Mali Ili Tu Uendelee Kuishi Kwenye Jahanam Ya Dunia"

"Wanawake Wenzangu Hakuna Neno Nimetoka Nae Mbali Au Nimechuma Nae Mali Acheni Utumwa Wa Akili Na Upofu Wa Mali, Furaha Huna, Amani Huna Yaani Duniani Haupo Na Akhera Unauliziwa, Amkeni Na Mjipiganie Kisha Msaada Utakukuta Mbele Kwa Mbele" amesisitiza @batuliactresstz na kumalizia kwa kusema

"Huyu Dada Anahitaji Msaada Mkubwa Sana Sio Kubezwa Wala Kuzomewa Kifupi Huyu Ni Shujaa Haswa 👏🏽💪🏽 Queen"

Queen ambaye anajishughulisha na utengenezaji wa keki, imeelezwa yeye na Dr.Mwaka wameishi pmoja takribani miaka 10 huku wakiwa wamejaaliwa watoto wawili

Queen amesema kwa hatua aliyofikia mali sio muhimu kwake bali anataka talaka yake awe na maisha yake mengine yenye amani badala ya vitisho na kukosa uhuru juu ya maisha yake hata hivyo Dr.Mwaka anaonekan ahayupo tayari kutoa talaka sababu haijawa wazi

Post a Comment

0 Comments