Khalid Aucho: Nipo Fiti, Nawataka Real Bamako Uwanja Wa Mkapa, Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Khalid Auch

KIUNGO mkabaji wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho, ameshusha presha kwa mashabiki wa timu hiyo, baada ya kusema kwamba, yupo fiti kuwavaa wapinzani wao, Real Bamako.


Mganda huyo alishindwa kumalizia mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D dhidi ya Real Bamako uliochezwa Mali na kumalizika kwa bao 1-1, baada ya kuumia.


Akizungumza na Soti Xtra, Aucho alisema yupo tayari kucheza mchezo dhidi ya Real Bamako utakaochezwa Machi 8, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar, kama kocha akihitaji kumtumia.


Aucho alisema kuwa anafahamu umuhimu wa mchezo huo, huku akiwashukuru madaktari wa timu hiyo, kwa huduma ya kwanza aliyoipata uwanjani kabla ya kurejea Tanzania kuendelea na matibabu.


“Ninaendelea vizuri hivi sasa baada ya kupatiwa huduma ya kwanza palepale uwanjani, kisha baada ya hapo matibabu yaliendelea.


“Awali madaktari walidhani nimepata jeraha la goti, lakini baada ya kunifanyia vipimo nikaonekana nipo vizuri isipokuwa nina michubuko tu chini ya goti.


“Nipo tayari kucheza mchezo ujao dhidi ya Bamako watakapokuja nyumbani, kama kocha akinihitaji kunitumia, hivyo mashabiki wa Yanga waondoe hofu,” alisema Aucho.


STORI NA WILBERT MOLANDI

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad