Ticker

6/recent/ticker-posts

Mashabiki Watengeneza Album Feki ya Davodo....Wizkid na Ali Kiba Ndani Kwenye Collabo

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Inawezekana nyota wa muziki kutokea nchini Nigeria, Davido akawa ni mmoja ya wasanii waliobahatika kupata mashabiki kindakindaki zaidi ulimwenguni.


Nyota huyo amejikuta akitengenezewa ‘Album’ feki na mashabiki zake huku wengi wakiendelea kulilia ujio wake tena kwenye muziki.


Watu hao wasiojulikana wameipa jina la “Imagination wanna kill me” Album hiyo feki, huku ndani yake kukiwa kuna jumla ya ngoma 17.


‘Tracklist’ ya album hiyo feki, imejumlisha kolabo mbalimbali nje na ndani ya Nigeria huku kukiwa na wimbo aliomshirikisha Wizkid

kutokea Nigeria (Dey Play ambayo ni track namba 15) na nchini Tanzania wakimuweka msanii @officialalikiba kwenye track namba 10 waliyoipa jina la “Let’s Go”.


Uongozi wa Davido haujatoa neno lolote kuhusiana na Album hiyo ila wapo wanaoamini kuwa labda nyota huyo yupo mbioni kuja na album nyingine mara baada ya kufuta ‘post’ zake kwenye mtandao wa Instagram.


Una maoni gani kuhusu hili?

Post a Comment

0 Comments