Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwana FA "Wasanii Warudishe Mikopo Waliyopewa Kwa Wakati"

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu @mwanafa amewataka Viongozi wa Wasanii kuwasimamia Wasanii waliopewa mikopo kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania kurejesha fedha hizo kwa wakati kwa kuzingatia mwongozo waliopewa wakati wa kukopeshwa ili na wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.


Amesema hayo Dar es salaam Leo March 11, 2023 alipotembelea Ofisi za Mfuko huo ili kufahamu shughuli mbalimbali wanazotekeleza.


Amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo kuhakikisha makundi yote ya Wadau wa Sanaa na Utamaduni yanazingatiwa katika utoaji wa mikopo kwa kuzingatia vigezo na masharti ya mikopo hiyo.


Katika hatua nyingine Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma amewasikiliza baadhi ya Wanufaika wa Mfuko huo wakiwemo Wasanii wa muziki, Wazalishaji wa filamu na Wabunifu wa mitindo na mavazi ambao walieleza namna ambavyo wamenufaika na mfuko huo.

Post a Comment

0 Comments