Watatu, Askari Washikiliwa Wakidaiwa Kuiba Mitambo IPTL Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Baadhi ya mitambo ya kampuni binafsi ya kufua umeme (IPTL) inadaiwa kuibiwa na watu wanne akiwemo askari Polisi aliyekuwepo lindo siku ya tukio.

Mitambo hiyo iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ilisitishwa kutoa huduma ya kuzalisha umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwaka 2013 baada ya kutoelewana kwa wahusika wa mkataba wa makubaliano.

Kulingana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Oysterbay jijini hapa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha tukio hilo.


“Tumezipata taarifa hizo na tunazichunguza katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa,” ameeleza kwa ufupi bila kufafanua kwa kina.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad