Wanne Mbaroni kwa Tuhuma za Mauaji ya Mfanyakazi wa Geita Gold Mine

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Geita. Milembe Seleman (43) Mfanyakazi wa kitengo cha Ugavi katika kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu (GGML) ameuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiojulikana.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Geita Berthaneema Mlay amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Aprili 26, 2023 Saa 1:00 asubuhi Mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala mkoani Geita.

Mlay amesema baada ya kulata taarifa ya kuuawa kwa mfanyakazi huyo walifika eneo la tukio na kukuta amefariki huku mwili wake ukiwa umekatwa maeneo mbalimbali ikiwemo kichwani, usoni na mikononi ambapo kiganja kimoja cha mkono kiliondolewa.

“Kwa mujibu wa polisi waliofika kwenye tukio wanasema alikuwa amekatwa sehemu za kichwani usoni na kwenye mikono yote miwili ambapo mkono wa kulia kiganja kiliondolewa kabisa hayo ndio maeneo yaliyojeruhika zaidi”amesema Mlay


Kwa mujibu wa Kamanda huyo, watuhumiwa wanne wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Ruben Renatus mkazi wa Mtaa wa Mwatulole amesema akiwa njiani kwenda kazini alipata taarifa ya mwili wa mwanamke kuwa ndani ya boma wa nyumba alizokuwa anajenga.

“Amefanyiwa ukatili mkubwa amechinjwa damu imetapakaa kwenye ukuta, tumeishirikisha polisi wakafika na kuchukua mwili tukio hili limetusikitisha mama huyu alikua anajenga nyumba kwenye mtaa huu na ni nyingi zingechangamsha mtaa wetu lakini wahalifu wameondoa uhai wake na kitendo hiki kinaweka doa kwenye mkoa wetu”amesema Renatus
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad