Mwanaume Akamatwa Akifanya Biashara ya Ngono Mwanza

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limemkamata kijana mmoja aliyekuwa akijiita jina la kike la Asmat Abdalah na kuacha jina lake halali la Isma Abdalah kwa lengo la kuwalaghai wanaume kuwa yeye ni mwanamke amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza.

Akizungumza na vyombo vya habari, leo Mei 12, 2023 Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema kijana huyo alikamatwa katika eneo la Bar maarufu ya Villa Park iliyopo Kirumba Ilemela Mkoani humo akiwa amepanga mstari akisubiri wanaume kwa lengo la kumnunua ili kuingiliwa kinyume na maumbile.

"Huyu kijana alikuwa akijiita jina la Asmat lakini yeye jina lake halisi ni Isma, huyu tumembaini wakati tunataka kumuweka katika sero ya wanawake, kabla ya kuwaweka sero lazima ukaguzi ufanyike na baada ya kumkagua tulibaini ana jinsia ya kiume,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Aidha Kamanda Mutafungwa ameeleza kuwa kijana huyo atafikishwa mahakamani kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad