Mzee Abdul : Mimi na Diamond Platnumz Tuko Vizuri Hatuna Shida

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mzee Abdul : Mimi na Diamond Platnumz Tuko Vizuri Hatuna Shida

Baba wa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Jumaa amesema kuwa yeye na mtoto wake huyo wapo vizuri na anamsaidia kama ilivyokuwa awali.

Ikumbukwe kuwa, miaka miwili iliyopita, familia ya mama Diamond wakiongoza na mama yake mzazi Bi Sanura au Sandra ilisema kuwa mzee Abdul sio baba mzazi wa Diamond kwani alikuwa mlezi tu na baba yake aitwaye Mzee Nyange alishafariki dunia miaka mingi iliyopita.

Jambo hilo liliibua maswali mengi huku Diamond na kaka yake Ricardo Momo wakithibitisha kuwa mzee Abudl si baba wa Diamond.

"Mimi na Diamond Platnumz tuko vizuri, bado ni mwanangu yeye anaitwa Naseeb Abdul mimi naitwa mzee Abdul, tuko vizuri hadi familia yake ingawa kuna kipindi nilikasirika baada ya mama yake kuleta mambo ambayo hayakuwa ya kweli.

"Diamond na Queen Darleen wote ni watoto wangu, sina shida nao na hata nikiwa na shida hawawezi kunitupa," amesema Mzee Abdul.

Aidha Mzee Abdul amesema ameacha kuimba muziki kwasababu umri wake haumruhusu, ameshachelewa hata akisema aimbe vipi hataeleweka, lakini moja ya vipaji alivyojaliwa na Mungu ni kuimba na kuigiza na hata watu wa Tamthilia za Juakali, Huba, Pazia na nyinginezo wakimuita yupo tayari na atafanya vizuri.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad