Shamsa Ford Adaiwa Kupora Mume wa Mtu, Jamaa Atelekeza Familia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Shamsa Ford Adaiwa Kupora Mume wa Mtu, Jamaa Atelekeza Familia

Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, kauli hii inakuja baada ya Mwigizaji Staa wa Bongomovie, Shamsa Ford kumuiba mume wa mtu na kummiliki mazima bila kujali kwamba Mwanaume huyo ana familia ya mke na mtoto mchanga.


Mwanamke husika ambaye ameibiwa mume anasema yeye na mume wake huyo ambaye pia ni Muigizaji (Mlilo) wamedumu kwa miaka minne na wana watoto wawili, mwanamke huyo amesema Shamsa Ford amefanikisha kumuibia mume wake na kumutenganisha mume na watoto wake bila huruma na kuishia kumuacha kwa kumpa talaka tatu.


"Adiu wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, kwahiyo mimi adui yangu mkubwa ni Shamsa, nataka niongee live watu wasikie, namchukia yule dada Mungu anisamehe, yani namchukia hapa duniani mpaka akhera, hata kama itatokea duniani tukabaki wawili nisingeweza kusemeshana nae yule dada"


Amelalamika kwa kuongeza kuwa anaamini mume wake amepumbazwa akili hajielewi kwani alikuwa anampenda sana, anaamini ipo siku akili ya mume wake itarudi atakuja kutambua alichokifanya siyo sahihi.


Kwa upande wa Shamsa Ford alipoulizwa kama ni kweli amemkwapulia mume mwanamke mwenzake, alijibu kuwa hamjui huyo mwanamke na wala hajawahi kuiba mume wa mtu.


Hata hivyo, Shamsa Ford na Hussein Lugendo (Mlilo) wamekuwa wakionekana kwenye sehemu mbalimbali za starehe na kupostiana kwa kusifiana huko Instagram kiasi kwamba huwezi kukataa pindi unapoambia kwamba ni mtu na mtuwe kwani dalili zote za kuwa wapenzi zilishaonekana tangu muda mrefu.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad