Header Ads Widget


BREAKING: Ajali Mbaya ya Magari yatokea Arusha, Vifo na Majeruhi, Wamo Wazungu


BREAKING: Ajali Mbaya ya Magari yatokea Arusha, Vifo na Majeruhi, Wamo Wazungu

Watu kadhaa wamefariki,wengine kujeruhiwa baada ya gari kubwa Scania kudaiwa kufeli break na kwenda kuparamia magari matatu aina ya coaster,Daladala,na gari nyingine ndogo katika eneo la Kibaoni Ngaramtoni,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha

Ombeni Kirusha shuhuda wa tukio hilo amesema….“Kilichotokea ni ajali,nilikuwa na gari ndogo nikapisha gari iliyobeba cartepilar ikaparamia magari hayo kulikuwa na magari matatu moja imebeba wazungu,hiace na Mercedes Benz nakusababisha vifo vya watu kadhaa, tumeokoa waliokuwa wanahema watu nane,nilioshuhudia wamefariki walikuwa zaidi ya kumi”Ombeni

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha bado halijatoa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo na tunaendelea kufuatilia ili kupata idadi ya vifo,majeruhi na walionusurika.


Post a Comment

0 Comments