Furaha ya Ushindi wa Yanga Yasababisha Ali Kamwe Kuzimia, Akimbizwa Hospitalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Wakati mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao baada ya kuichapa CR Belouizdad kwa mabao 4-0 hali sio nzuri kwa Ofisa habari wake, Ali Kamwe ambaye ameanguka na kupoteza fahamu baada ya mchezo huo kumalizika.

Kamwe amekumbana na hali hiyo leo Februari 24, 2024 wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambapo ameanguka na kupoteza fahamu.

Kamwe amechukuliwa na kutolewa nje vyumba hivyo kisha kupelekwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini, Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yupo kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo.

"Nikweli Kamwe amepatwa na tatizo la kupoteza fahamu tupeni muda tumsaidie kwa haraka ili arejee kwenye afya yake," amesema Sufian ambaye ni daktari wa zamani wa Yanga.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu ya Yanga wamethibitisha hilo na kuandika kuwa:-

“Wananchi, Afisa habari wetu @alikamwe alipata changamoto dakika chache kabla ya mchezo wetu kuisha na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan kupata matibabu.

Hivi sasa anaendelea vizuri na yuko salama salmin.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad