Rais was Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kuifunga CR Belouizdad bao nne kwa sifuri na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali, akisema mafanikio hayo yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini.
Rais Samia amenukuliwa akisema; “Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali. Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla.”
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA