Ali Kamwe Afunguka Sakata la SIMBA nao Kuomba Serikali Kusafirisha Mashabiki Mpaka Cairo Kama Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ali Kamwe
Ali Kamwe
Eti Tunapendelewa? Nafikiri Tukio la leo linapaswa kuwaamsha na kuwaonyesha mashabiki wa Makolo kuwa wana viongozi wa namna gani

Sisi Tulishaanza mchakato wetu wa safari mapema. Zaidi ya Mashabiki 30 walishalipia 600,000 zao za safari .. Uongozi ukaona kuna Fursa ya kuishirikisha Serikali kusaidia kidogo mashabiki wetu kwenye accommodation..

Bahati nzuri, Mungu ametujaalia Serikali yenye viongozi wenye upendo. Wakapokea ombi letu, wakapitia bajeti yetu .. Na kwa maslahi mapana ya Nchi, Wakaibeba Safari ya Mashabiki wetu

Ajabu, Makolo kwa mkurupuko mkubwa.. Kwa hoja za kitoto kabisa, wameibuka na kudai Eti na wao wasafirishwe na Serikali kama Yanga 😀

Hii inatafsiri katika mipango yao, hawakuwawaza mashabiki wao kwa Lolote kwenye hii safari. Walishawatelekeza.. Hakukuwa na Plan Yoyote kuhusu wao

Ila kwa sababu Yanga wamewaza na Jambo Limefanyika .. Basi nao kipele kikawawasha.

Na hii sio mara ya kwanza… Makolo wamekuwa wakitembelea njia ya Viongozi wa Wananchi hata kwenye ishu ya Mikataba kutoka Taasisi mbalimbali kwa kigezo ‘Sisi ni kama wao’

Mkome! Hamko Levo zetu na Hamtakaa mfike.

Uzembe wenu msitake kuwabebesha lawama viongozi wetu wa Serikali ambao kwa kipindi cha miaka hii miwili wamekuwa Bega kwa Bega kuhakikisha wanasaidia maendeleo ya Sekta yetu ya Michezo..

Mwisho niwashauri Mashabiki wa Makolo .. Rudini kwenye Mkutano Mkuu muwaulize viongozi wenu, Mliwachagua wacopy kwa Yanga jinsi ya kuengage Fans Au wako na Plan yoyote Tofauti kwenye vichwa vyao?

Mwenyekiti wa Wasemaji🧠
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad