Kocha Matola Atoa Kauli ya Kukata Tamaa "Kwa Hali Hii Ubingwa Kwetu Simba Mgumu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kocha Matola Atoa Kauli ya Kukata Tamaa "Kwa Hali Hii Ubingwa Kwetu Simba Mgumu"

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kwasasa mbio za ubingwa ni ngumu kwao lakini watapambana kumaliza vyema michezo iliyosalia.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Yanga uliomalizika kwa vijana wake kuvurugwa 2-1 kocha huyo amesema bado shida yao ya kushindwa kutumia nafasi inawatafuna.

“Kuhusu ubingwa kwa sasa naweza kusema ni ngumu kuupata lakini tunaangalia zaidi mechi zilizosalia kuona tutapata nini,” amesema Matola.

Mchezo wa mwisho walipokutana katika dabi ya Kariakoo Novemba 05, 2023 Simba SC walifungwa 5-1. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 58 baada ya michezo 22 huku Simba wakisalia na alama 46 kwenye nafasi ya tatu.

Simba kesho itamenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano, Uwanja wa New Amaan Complex visiwani, Zanzíbar wakati Azam FC itaanza na KMKM Alhamisi na Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad