MULIRO: Malisa GJ, Boniface Jacob Wakamatwe Kwa Tuhuma za Kupotosha Taarifa za Kifo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MULIRO: Malisa GJ, Boniface Jacob Wakamatwe Kwa Tuhuma za Kupotosha Taarifa za Kifo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne amesema wanatarajia kuwashikilia Malisa GJ na Boniface Jacob kwa madai ya kusambaza taarifa za uongo katika Mitandao ya Kijamii kuhusu kifo cha Robert Mushi “Babu G”. Amedai wametengeneza taharuki kwa Wananchi na chuki dhidi ya Polisi na Serikali


Muliro amesema Babu G alipata ajali ya kugonjwa na gari ambalo halikusimama wakati akivuka Barabara maeneo ya Buguruni, Ilala, Aprili 11, 2024, Saa 10 Alfajiri na kupata majeraha makubwa Kichwani, Kifuani, Chini ya Mgongo na Kisigino cha Mguu wa Kulia


Amesema eneo ilipotokea ajali lina Watu wengi ambao wanakesha kwa biashara mbalimbali na walishuhudia tukio husika, pia ameeleza kuwa Polisi walifika na kumpeleka majeruhi Hospitali ya Amana. Alipofikishwa Madaktari walibaini alikuwa ameshafariki, kutokana na kujaa kwa chumba cha kuhifadhi maiti, mwili ulipelekwa Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyo Barabara ya Kilwa Temeke


Ameongeza kuwa mwili haukutambulika kwa kuwa hakuwa na Kitambulisho wala Simu, ndipo Aprili 21, 2024 ndugu wa marehemu walipatikana na kuutambua mwili na taratibu za mwisho za mazishi zinafanywa ili akazikwe


#JFMatukio #JamiiForums

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad